MTUME NYAGA HR

AGALIA EMMANUEL TV LIVE [WATCH EMMANUEL TV LIVE]

Alhamisi, 18 Aprili 2013

WASILIANA NA MTUME PETER NYAGA WA KANISA LA RGC TABATA CHANG'OMBE


MTUME PETER NYAGA AGUSA MIOYO JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA SEMINA YA WAJASIRIAMALI


MTUME PETER NYAGA WA KANISA LA RGC TABATA CHANG'OMBE AGUSA MIOYO YA WATU JIJINI DAR ES SALAAM

Kutoka RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe

Mtume Nyaga agusa moyo wa jamii Dar

Mitume Manabii watikisa jiji wiki hii

Ishara, maajabu na miujiza vyatawala madhabahu ya RGC

Wengi wapiga kambi kanisani kuwahi vipindi


Katika hali isiyokuwa ya kawaida viti ndani ya ukumbi wa kanisa la RGC Miracle centre Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu vimekuwa vikikosa mkaliaji kutokana na wahudhuriaji kusikiliza mahubiri wakiwa wamesimama kwa sababu ya upako unaotawala ndani ya nyumba hiyo ya ibada wakati wa kongamano la kihistoria la siku 40 linaloendelea ndani ya kanisa hilo.

Licha ya kongamano hilo la kihistoria kuchukua muda mrefu, lakini idadi ya watu wanaomiminika kanisani hapo kuhudhuria kongamano imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hali ambayo imekuwa ikiwashangaza wengi.

Mbali na ishara, miujiza na maajabu kutawala eneo hilo, jambo jingine ambalo limeonekana kuwavutia na kuwashangaza wengi ni hatua ya kiongozi wa kanisa hilo mtume Peter Nyaga, kuamua kuanzisha program maalum ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo imeonekana kuvuta watu wengi hasa wenye kipato cha chini na wasio na ajira .

Wengi waliohudhuria mafunzo hayo walimshukuru na kumsifu mtume Nyaga, kwa ubunifu wake kwani wanaamini pindi watakapofika mwisho wa mafunzo hayo ya siku 40 yatakuwa msaada mkubwa katika maisha yao. Walisema hii ndiyo sababu iliyowafanya wengi wao kuamua kuhama majumba yao na kupiga kambi kanisani hapo ili kuhakikisha hawakosi kipindi hata kimoja.

Tangazo limetengezwa na RUMAFRICA

Jambo jingine lililosifiwa na wahudhuriaji mbali na mafunzo ya ujasiriamali ambayo yanaonekana kuwakomboa wengi tangu yalipoanza ni hatua ya mtume Nyaga, kuwaleta watumishi wa Mungu kutoka madhehebu tofauti kwa ajili ya kuwahudumia kiroho baada ya mafunzo ya ujasiriamali jambo ambalo walisema ni la kipekee hasa katika kipindi hiki ambapo ushirikiano miongoni mwa watumishi wa Mungu unaonekana kupungua nguvu.

Pia katika kuendeleza kuboresha maisha ya watu wanaobahatika kuhudhuria kongamano hilo la kihistoria, wiki hii mtume Nyaga, amealika wataalam wa afya kutoka nchini Malaysia ambao watafundisha nguzo nne muhimu za kuishi maisha mazuri na yenye afya bora.

Je unajua magonjwa haya yanasababishwa na nini mwilini mwako?

*Saratani ya utumbo mkubwa
*Vidonda vya tumbo
*Shini kizo la damu |
*Kisukari |
*Kufunga na kukosa choo mara kwa mara
*Figo kushindwa kufanya kazi vizuri
*Matatizo ya moyo
*Kukua kwa tezi ya prostrate (Prostrate gland)
*Kihararusi/Stroke
*Ngiri
*Magonjwa ya ngozi
*Unene uliopindukia
*Lehemu/ Cholesterol
*Harufu mbaya mdomoni na kikwapa

Usikose RGC Miracle Centre wiki hii, kwani wataalam hawa waliobobea watakufundisha namna ya kuwa na afya bora huku watumishi mbalimbali wenye upako wakikuombeea na kukufungua kutoka katika vifungombalimbali vya shetani vilivyokutesa kwa muda mrefu.


Ijumaa, 12 Aprili 2013

KONGAMANO LA SIKU 40 ZA KIHISTORIA ZA UDHIHIRISHO WA HUDUMA TANO GRC TABATA CHANG'OMBE




Limetengenezwa na Rumafrica
www.rumaafrica.blogspot.com
www.rumaafricajobs.blogspot.com
Simu: +255 715 851523
Sinza Afrika Sana, Dar es Salaam, Tanzania

NTUME NYAGA AFANYA MKUTANO WA INJE- LAWITI

Mtume Peter Nyaga akihibiri
Mtume Peter Nyaga
 Watu wakiwa katika maomb




 Watu wakipokea baraka za Mungu




Kama ilikawaida ya blog yangu hii hua ina kuleta mambo yangu na mambo mengine yanayo husu jamii bila ya kusahau gospel yaani wasanii wa nyimbo za Ijili. Hii haijawahi kutokea hapa kisiwani watu kuhudhuria katika mkutano wa ijili kama hivi. kwakweli wasanii tupo juu maana wasanii wa nyimbo za injili wamekiteka kisiwa hiki kwa kumiminina watu katika uwanja wa tumbatu uliopo hapa Zanzibar. JOSUPH NYUKI, NEEMA MWAIPOPO na JANE MISSO wame ikama ta Zanzibar wakifuanata na mtume PETER NYAGA.

umati wa watu ulio kusanyika katika mkutano huu ambao ulifanyika kuanzia tarehe 21-23mwezi huu huu wa kumi mwaka 2011

jamani hii ni Zanziamakweli mambo yana badilika

picha hii nilipigwa kwa kustukizwa maana nilikua mshamba kwa kuona umati kama huu kwangu ilikua ni ajabu kwa mambo haya kutokea kisiwani hapa.
mtume Nyaga akiwaombea watu.
mzee akitoa mambo kwa msisitizo
mtume Nyaga ndo huyu hapa akiwa jukwaani Zanzibar
Mtume Peter Nyaga akihubiri

IKAFIKA ZAMU YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA IJILI YAANI WASANII
tutake tusitake wasanii tuna hitajika tu maana licha wa mahubiri watu pia wali fuata wasanii wa nyimbo za ijili ndio maana uwanja ukajaa hivyo na kwakweli walitenda haki
Neema Mwaipopo na Jane Misso wakipagawisha watu jukwaani

Mwaipopo akiwaimbia "Jamani rahaaaa jipemwenyeweeeeee" ilikua sio mchezooo
Jane misso akirudi kukaa
waandishi wa habari pia walikuwepo
kitu kilikwenda mpaka usiku hapa Nyuki ndo alisimama kwa ajili ya kuimba watu walipiga kelele na wengine kukanyagana kwaajili ya kuona manjonjo ya huyu bwana. kama huja wahi kumuona jukwaani basi pole na utakapo muona uniambie. kweli sanaa ni kipaji toka mouoni
akianza manjonjo
haya atayari ana anza huyooo
ilikua tayari usiku ila watu walikomaa kuangalia shoo hao ni baadhi ya wachungaji na huyo mwenye suti nyeupe ni Askofu wa makanisa ya kipentekoste Zanzibar Bishop: Obeid.weweeeee

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...