Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20)
Maombi ya
vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba
Maombi haya
ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na
kuomba. (Ombi la tano 5). Kumbuka
maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla
ya kulala na baada ya kuamka.
Maombi ya
kupinga magonjwa, vifo, ajali na uharibifu
1. Baba,
katika jina la Yesu, naangusha kila mbinu za kishetani zinazozuia mafanikiao
yangu, katika jina la Yesu.
2. Nakataa na
kupinga magonjwa ya kila aina katika nyumba yangu na familia yangu, kwa jina la
Yesu.
3. Imeandikwa katika
Zekaria 2:8 ya kwamba “Yeye
anayenigusa mimi anagusa mboni ya jicho la Mungu”, hivyo, ninalisimamia
Neno hili na kupinga kila nguvu inayosababisha magonjwa na upotevu wa fedha
zangu katika jina la Yesu.
4. Nasimama
kinyume na ajali na vifo katika familia yangu na ndugu zangu katika jina la
Yesu.
5. Nawafunika
watu wa familia yangu, kijiji changu na nje ya kijiji kwa damu ya Yesu.
Ninawalinda na kuwaongoza kila mmoja kwa jina la Yesu.
6. Ninaamuru
kila kinachoharibu mtaji na biashara yangu kufa mara moja katika jina la Yesu.
7. Ninaificha
fedha yangu yote katika damu ya Yesu na kamwe adui hawezi kuigusa.
8. Baba, katika jina la Yesu, nasimama katika Neno
kama mtoto wa Mungu niliyeketishwa mahali pa juu pamoja na Kristo, na
ninatangaza kuwa mikutano ya kipepo juu ya maisha yangu na fedha yangu
haitafanikiwa, katika jina la Yesu.
9. Namfunga kila anayeharibu fedha yangu nyumbani
na sehemu yangu ya kazi katika jina la Yesu.
10.
Wewe pepo
uliyetumwa kuharibu biashara na fedha zangu, ninakufunga na kukutupa kwenye
shimo la giza katika jina la Yesu.
11.
Ninaamuru moto
wa Roho Mtakatifu kumlamba kila mmoja aliyesimama kinyume na biashara na
mafanikio yangu katika jina la Yesu.
12.
Ewe mlima
uharibio, ninakuangusha na nianaamuru usambaratike, katika jina la Yesu.
13.
Ninaificha
biashara, ofisi, fedha na miradi yangu yote katika damu ya Yesu Kristo Mwana wa
Mungu aliye hai. Amen.
14.
Bwana, ninaomba
upendeleo wako katika maisha yangu ili niweze kufanikiwa.
15.
Upendeleo wako
unizunguke kadiri ya Neno lako, katika jina la Yesu.
16.
Bwana, naomba
kuunganishwa na watu watakaonisaidia kufikia ndoto zangu kwa jina la Yesu.
17.
Oh, Bwana,
naomba ufanye njia kwa ajili yangu hata pale pasipo na njia katika jina la
Yesu.
18.
Baba, naomba
niunganishe na mtu ambaye atakuwa msaada mkubwa katika kuyafikia mafanikio
yangu katika jina la Yesu.
19.
Baba ninaamini
ya kwamba kila ninapokanyaga ninapamiliki sawasawa na na Neno lako, hivyo
naomba univike vazi lako la upendeleo katika jina la Yesu.
20.
Asante Bwana
Yesu kwa kuwa umefanya sawasawa na nilivyokuomba katika jina la Yesu. Amen.
Baada ya
kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu
Usikose
Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja
maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa
la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya
Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa
lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana.
Kwa
mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011
Mimi wako
Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe
-------------------------------------------------------------------------
Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20)
Maombi ya
vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba
Maombi haya
ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na
kuomba. (Ombi la
Sita 6). Kumbuka maombi
haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla ya
kulala na baada ya kuamka.
Maombi ya
kubariki kazi za mikono yetu
1. Mungu wa
milele yote “Niko ambaye niko” ninakuabudu na kukutukuza. Uhimidiwe katika
jina la Yesu.
2. Bwana, nainua
kazi yangu na kuikabidhi kwenye mikono yako.
3. Nawakabidhi
wafanyakazi wenzangu na mkubwa wangu wa kazi mikononi mwako. Nipe upendeleo
wako mbele yao wote katika jina la Yesu.
4. Imeandikwa
katika Isaya 45:2 kwamba “utakwenda
mbele yangu na kupasawazisha penye matatizo” kwa hiyo, nakuomba uniandalie
njia ya kuinuliwa katika ofisi yangu, katika jina la Yesu.
5. Imeandikwa
katika Zaburi 1:3 ya kwamba lolote
nitakalolifanya litafanikiwa. Hivyo, Baba nifanye ning’ae katika kazi yangu ili
niweze kupandishwa cheo katika jina la Yesu.
6. Baba, nachukua
mamlaka dhidi ya falme, mamlaka na nguvu zote za giza katika ofisi yangu,
Ninawafunga na kuharibu nguvu zao zote katika jina la Yesu.
7. Wewe pepo
wa ukabila ninakufunga na kukutupa nje ya maisha ya bosi wangu na waajiri wote katika jina la Yesu.
8. Kila nguvu
za giza katika eneo langu la kazi ambazo hutaka mimi nifukuzwe kazi,
ninaziharibu na kuzifuta kabisa katika jina la Yesu.
9. Baba naomba
ustawi katika biashara zangu zote katika jina la Yesu.
10.
Ninakataa kila namna ya udanganyifu na wizi
katika eneo langu la kazi.
11.
Bwana, nibariki na kunipa upendeleo katika
maisha na kazi zangu kwa jina la Yesu.
12.
Imeandikwa “matamanio
ya mtu mwema yatatimizwa”. Hivyo, Bwana Yesu nipe matamanio ya moyo
wangu katika jina la Yesu.
13.
Kila nguvu za
giza zilizosimama kinyume nami kuzuia kuinuliwa kwangu na kupandishwa cheo,
ninaziharibu na kuziondoa katika jina la Yesu.
14.
Wewe pepo
unayesimamisha na kurudisha nyuma maendeleo yangu, ninakufunga na kukutupa nje
ya kazi yangu na maisha yangu katika jina la Yesu.
15.
Bwana,
ninaikabidhi biashara yangu mikononi mwako, naomba uitawale, katika jina la
Yesu.
16.
Bwana, niongoze katika kuitumia pesa yangu na kujua
maeneo ya kufungua biashara katika jina la Yesu.
17.
Bwana, nipe
hekima ya kuendsesha biashara ili niweze kufanikiwa na kustawi katika jina la
Yesu.
18.
Bwana, naomba
upendeleo wako kwenye bidhaa nitakazoziuza ili zipate kibali machoni pa watu
katika jina la Yesu.
19.
Nisaidie kujua
mazingira yangu na kuweza kugundua kazi au biashara unayotaka mimi niifanye ili
niweze kufanikiwa katika jina la Yesu.
20.
Baba,
ninakabidhi fedha zangu zote mikononi mwako, katika jina la Yesu.
21.
Bwana ingilia
kati na unipe Baraka na hekima ya kufanya biashara itakayozalisha kwa wingi. Amen.
Baada ya
kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu
Usikose
Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja
maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa
la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya
Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa
lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana.
Kwa
mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011.
Mimi wako
Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe.
--------------------------------------------------------------
MWAMINI
MUNGU UTHIBITIKE, AMINI NABII UFANIKIWE (2 NYAKATI 20:20)
Maombi ya
vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba: Ombi la tatu. Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila
wiki ni siku 1 tu ya kufunga na kuomba (Ombi la Tatu 3).Kumbuka maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni
vema kufanya maombi haya kabla ya kulala na baada ya kuamka
Jinsi ya kuomba maombi ya kuugua na
kulia
Sio rahisi
kabisa kuomba maombi ya kuugua na kulia, hata tunapoomba mambo ya rohoni kama
uamsho, watu wote waokolewe, Bwana azidi kumtumia vema mchungaji , kuombea
ibada ya siku ya matendo makuu ya miujiza, mkutano wa injili nk.Ni rahisi
kufanya maombi ya kulia na kuugua hasa tunapomwomba Mungu atuponye magonjwa yetu mabaya, atupe kazi
kimiujiza, ashughulikie mume/mke anayetutesa nk. lakini sio rahisi tunapoombea
mambo ya rohoni kama ifuatavyo.
Kutiisha mwili
Miili yetu ni
rahisi sana kulia na kuugua tunapopata msiba au mateso ya kimwili, lakini
linapokuja suala la kulia na kuugua kwa mambo ya rohoni, miili yetu hupingana
nasi kabisa na kutufanya tusione maana ya kulia na kuugua katika maombi ya
jinsi hiyo, pamoja na shetani kuwa adui yetu mkuu, miili yetu pia ni maadui
zetu wakubwa wanaopingana na kila jambo la rohoni tunalotaka kulifanya Wagalatia 5:17 na kwa sababu mwili hutamani
ukishindana na roho na roho hushindana na mwili kwa maana hizi zimepingana hata
hamuwezi kufanya mnayotaka.
Hatuna budi kuutiisha
mwili ili tufanye mambo ya rohoni kinyume na hiyari yake (Warumi 8:6-8;19-21; 2Wakorintho10:4-5). Tukiunganisha mawazo na
kila kitu kilichoinuka, kiinukacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka kila fikra
ipate kumtii Kristo. Kwa hiyo kabla ya kuingia katika maombi ya rohoni ya
kuzama kwa kina yaani ya muda mrefu, ambayo tunataka yawe ya kulia na kuugua,
sharti tuutiishe mwili na kuuamuru kuwa
chini ya roho zetu na kukemea kila mipango ya shetani ya kutuzuia kuomba kwa
kuugua.
Kuomba tupewe roho ya neema ya kuomba
Hatuwezi
kufanya maombi ya kuugua na kulia mpaka pale tunapopewa au kumwagiwa roho ya
neema na kuomba Zakaria 12:10, “nami
nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na
kuomba nao watamtazama yeye ambaye walimchoma, nao watamuombolezea kama vile
mtu amuombolezeavyo mwanawe wa pekee nao wataona uchungu kwa mzaliwa wake wa
kwanza”.Hivyo baada ya kuutiisha mwili, hatuna budi kuwa na kipindi cha
kutosha kuomba tumwagiwe roho ya neema na kuomba, kipindi hiki hakina budi
kuchukua muda upatao dakika 20, na kile cha kwanza cha kutiisha mwili hakina
budi kuchukua muda upatao dakika 10. Baada ya dakika hizi ndipo tunaweza kuomba
maombi yanayoweza kumfanya Mungu ashuke, hata hivyo kuna utata kidogo. Je roho
ya neema ni nini?
Roho ya neema na kuomba
Kwanini hatuna
budi tumwagiwe roho ya neema? Ili tujue ni kwa nini hatuna budi kuelewa na
kujikumbusha maana ya neema, kwa ufupi na kwa urahisi wa kuelewa ni msaada utokao mbinguni wa kutuwezesha
kufanya yale ambayo tusingeweza kufanya kwa nguvu au jitihada zetu wenyewe (Waebrania 4:16; 1Wakorintho 15:10) “basi
na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema
ya kutusaidia wakati wa mahitaji”.Kwa msingi huu wanadamu wote ni dhaifu
sana katika maombi ndio maana wengi utawasikia wakisema NAPENDA SANA KUOMBA LAKINI NAJIKUTA SIWEZI KUOMBA nitakavyo. Roho Mtakatifu
yeye hana tatizo hilo tulilonalo, la kushindwa kuomba, ni mwombaji wa kipekee
kama alivyo Yesu. Huyu ndiye msaidizi wetu Yohana
14:26. “lakini huyo msaidizi huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina
langu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia kwa kuwa yeye ni
mwombaji asiyefananishwa, hutupa roho ya
neema au roho inayotusaidia udhaifu wetu na kutufanya tuombe jinsi
inavyotupasa kuomba” . Bila roho hiiiya neema au ya msaada huu sisi
hatuwezi kuomba itupasavyo (Warumi 8:26)
“kadhalika roho naye hutusaidia udhaifu
wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo lakini roho mwenyewe hutuombea
kwa kuugua kusikoweza kutamkwa “
jitihada zetu pekee haziwezi kumlazimisha Mungu ashuke.
Roho ya kuomba
Roho ya
kuomba ni roho inayomwagwa kwetu na kutuwezesha kuomboleza au kulia na kuugua
katika maombi (Zekaria 12:10) “nami
nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na
kuomba nao watamtazama yeye ambaye walimchoma, nao watamuombolezea kama vile
mtu amuombolezeavyo mwanawe wa pekee nao wataona uchungu kwa mzaliwa wake wa kwanza”Roho
Mtakatifu huomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, hutupa neema au msaada wa
kutuwezesha sisi nasi kuomba kwa kulia na kuugua kunakoweza kumfanya Mungu
ashuke. Bwana atupe neema ya kuyakumbuka haya na kuyatendea kazi kabla ya
maombi marefu. Hakika tukifanya hivyo tutamwona Mungu akishuka kati yetu (Yohana 13:17).“mkiyajua haya heri ninyi mkiyatenda” tegemea kupokea upako huu
wa neema maishani mwako. Ni
matumaini yangu neno hili litakaa
ndani ya moyo wako na utalifanyia kazi. Kumbuka siri kubwa ya kuhifadhi maombi maishani
mwako ni kuogopa kutenda dhambi na kuacha dhambi kabisa Yohana 15:7; Kumb. 28:1-2. Tia bidii kusikiliza neno na kulitendea
kazi.
Maombi
1.
Baba
katika jina la Yesu natubu dhambi zangu zote leo, pia naomba uweza wa Roho
Mtakatifu unisaidie ili nisirudie tena.
2.
Bwana
Yesu nakuja tena kwako wewe Bwana wa msamaha ili nipate kusamehewa dhambi zangu
zote nilizorithi na kufanya, baba unisamehe (tamka dhambi ulizofanya, chukua
kama nusu saa ni bora zaidi).
3.
Baba
najiachilia kwa damu yake Yesu damu takatifu, damu iliyomwagika kalvari, damu
ya thamani, damu ya ushindi, damu ya uweza wa kumiminika juu yangu, na
kunitakasa katika jina la Yesu Kristo.
4.
Wewe
Yesu umesema, njooni kwangu ninyi wenye dhambi, wenye mizigo nitawapumzisha (Mathayo11:28). Bwana Yesu naja mbele
yako unipe pumziko nimechoshwa na maisha ya dhambi, na maisha ya kuanguka.
5.
Unisafishe
Bwana, sikia kilio changu mimi mkosefu nakuja kwako sasa nipokee kama nilivyo.
6.
Ee
Bwana Yesu wewe umejaa neema na rehema tele, chunguza nafsi yangu, chunguza
mwenendo wangu ili upate kunisamehe.
7.
Unishike
mkono wako Bwana, ukiniacha peke yangu nitaanguka maana shetani ananitafuta kwa
kasi sana usiku na mchana, Bwana nahitaji msaada wako kwa haraka sana tena sasa
hivi.
8.
Mungu
wa mbinguni naomba usamehe dhambi za babu zangu, Bwana unifundishe kila siku
kusamehe walionikosea na kuanzia leo nawasamehe kwa moyo wangu wote
walionikosea, kwa mabaya yote waliyonitendea, baba nawasamehe nakuomba pia
uwasamehe katika jina la Yesu Kristo.
9.
Bwana
Yesu kama maandiko matakatifu yashuhudiavyo, katika kitabu cha Isaya 59:1-3 naamini sasa na pia najua
ya kwamba mkono wako si mfupi kushindwa kuniokoa, wala wewe si kiziwi usisikie
ila maovu yangu yameufanya uso wako ugeukie upande mwingine, Bwana naomba
uniangazie ili nipate kupenya kimaisha na kupata wokovu wa milele katika jina
la Yesu Kristo wa Nazareti.
10. Bwana Yesu nakushukuru kwa kusikia kilio
changu, nakushukuru kwa kunisamehe
dhambi zangu zote, nakushukuru kwa kuwasamehe walionikosea, nakushukuru sana
kwa kunikubali tena, kwa kunipokea katika mikono yako mitakatifu, jina lako
lizidi kuinuliwa katika jina la Yesu Kristo.
11. Ubarikiwe Bwana wa majeshi uinuliwe mara saba kwa
mara sabini, jina lako lizidi kuabudiwa kila siku mahali popote.
12. Nakuja kinyume na falme na mamlaka zilizo
kinyume na harusi yetu katika jina la Yesu.
13. Nafunga kila pepo lililoandikwa kufunga ndoa
yetu katika jina la Yesu. Baba ifanye harusi yetu kuwa yenye mafanikio. Pokea
utukufu katika jina la Yesu.
14. Ngome ya moto inizunguke popote niendako
katika jina la Yesu.
15. Baba Mungu mbingu na ifunguke mvua ya neema
inyeshe Baraka za rohoni zinifikie mahali popote nipatikanapo katika jina la
Yesu Kristo.
16. Asante Mungu baba na Bwana Yesu kwa ajili ya
neema na rehema zako kwa kunijibu maombi yangu haya katika jina la Yesu Kristo
ninaomba. Amen
Baada ya
kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu
Usikose
Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja
maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa
la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya
Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa
lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana.
Kwa
mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011
Mimi wako
Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe
Mwanamaombi
namba ………………
--------------------------------------------------------------------------------------------
Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20)
MAOMBI YA
VITA YA SIKU 21 ZA KINABII ZA KUFUNGA NA KUOMBA
Maombi haya
ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na
kuomba. (Ombi la nne 4). Kumbuka
maombi haya hutolewa nakala mpya kila wiki. Ni vema kufanya maombi haya kabla
ya kulala na baada ya kuamka
Maombi ya
kuvunja laana za Umaskini
1. Katika jina
la Mungu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, ninavunja kila laana ya Baba na mama
yangu iletayo umaskini maishani mwangu, katika jina la Yesu.
2. Ninakataa
kuteseka na umaskini maishani mwangu kutokana na laana za wazazi katika jina la
Yesu. Amen.
3. Leo kwa
uweza wa Mungu aliye juu ninavunja kila aina ya laana ya umaskini maishani
mwangu kwa jina la Yesu.
4. Kama ilivyoandikwa
katika Mathayo18:18 natangaza katika
maisha yangu ya kwamba umaskini sio sehemu yangu katika jina la Yesu.
5. Mungu wangu
nifanye nisione umaskini wala kunukia harufu yake katika maisha yangu na
familia yangu kwa jina la Yesu.
6. Sikubaliani
na roho ya umaskini na kamwe haitaambatana nami wala familia yangu katika jina
la Yesu.
7. Napokea
upako wa Roho Mtakatifu na laana za wazazi kamwe hazitanifanya kuwa maskini
katika jina la Yesu. Amen.
8. Mungu wangu
na Bwana wangu, navunja kila laana na vyama vya siri walivyoninyunyizia kwa
jina la Yesu
9. Chochote ambacho wazazi wangu na marafiki walikifanya
kupitia vyama vya siri na wachawi nakivunja kwa jina la Yesu.
10.
Uchawi wowote
wa manuizo, maeneo waliyonilaani na kuniita nijiunge nao, nayadhoofisha na kuyaangamiza
kwa jina la Yesu. Amen.
11.
Roho chafu na
mapepo yanayoshughulika na chama cha wachawi na kazi zao ninazivunja jina la
Yesu. Amen.
12.
Ile laana ya
utasa maishani mwangu, na katika familia yangu naivunja katika jina la Yesu.
13.
Laana za utasa
wa utajiri, watoto na biashara nazivunja kwa jina la Yesu
14.
Navunja laana za utasa maishani mwangu,
nilizorithi kutoka kwa wazazi wangu katika jina la Yesu.
15.
Ninajiweka huru
mimi na familia yangu yote kutoka katika laana za utasa, nilizolaaniwa na
maadui kwa jina la Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.
16.
Adui wa afya njema kwa familia yangu
nakuvunja, nakufunga minyororo na kukuharibu kwa jina la Yesu.
17.
Navunja laana za utasa maishani mwangu. Nilizorithi
toka kwa wazazi wangu kwa jina la Yesu.
18.
Najiweka huru
mimi na familia yangu yote kutoka katika laana za utasa ambazo maadui walinilaani
nazo kwa jina laYesu.
19.
Utasa katika
familia yangu uwe umetoka kwa marafiki zangu, au walionitakia mema, ninauharibu
sasa kwa jina la Yesu.
20.
Laana zote za
utasa katika biashara kutoka kwa shetani nazivunja sasa na zisirudi tena katika
jina la Yesu.
21.
Laana ya utasa
kwenye maisha yangu, familia yangu, biashara na vinginevyo iwe imetoka kwenye
maroho machafu, watu, sehemu ninayoishi au kazini kwangu, naivuinja na kuilaani
sasa kwa jina la Yesu Amen.
22.
Laana za utasa
katika familia yangu na mababu zangu nazikataa sasa na kuzivunja kwa jina la
Yesu. Amen
Baada ya
kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu
Usikose
Jumapili hii saa mbili asubuhi. Itakuwa ni ibada maalum ya Urejesho na kuvunja
maagano mbalimbali maishani mwako. Ibada hii maalum itafanyika ndani ya Kanisa
la RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe. Jinsi ya kufika, Panda magari ya
Segerea, shuka Barakuda, pandisha na barabara iendayo Tabata Chang’ombe. Kanisa
lipo Chang’ombe mwisho kituoni. Hakika hapo Mungu anaonekana.
Kwa
mawasiliano, maombi na ushauri 0765-111011
Mimi wako
Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
MAOMBI MAALUM YA VITA YA KIL;A WIKI
OMBA KILA SIKU MAOMBI HAYA YA
KINABII
Mwamini Mungu uthibitike, Amini Nabii ufanikiwe (2 Nyakati 20:20)
Maombi ya vita ya siku 21 za kinabii za kufunga na kuomba (Ombi la pili
2)
Maombi haya ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 kila wiki ni siku 1 tu ya
kufunga na kuomba. Hakikisha umekuja kupakwa mafuta ya upako ili upokee neema
ya Mungu. Siku ya kufunga ni tarehe …………………………… Njoo saa moja asubuhi. Soma
maandiko haya kabla ya maombi. Amen
Kumbukumbu 28:1-14;
“Itakuwa utakaposikia sauti ya
BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo
leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;”
Nehemia 13:2, Luka 18:1; Isaya 43:18-19;
1. Baba wa
mbinguni katika jina la Yesu Kristo naomba
2. Baba wa
mbinguni jina lako litukuzwe duniani kama huko mbinguni katika jina la Yesu
Kristo wa Nazareti Mwana wa Mungu aliye hai.
3. Nakushukuru wewe Simba wa Yuda kwa kunipatia
nafasi katika siku hii ya tatu ya maombi yangu kwa njia ya vita vya kiroho,
jina la Bwana libarikiwe sana.
4. Ahsante kwa
kunitia nguvu tangu siku ya kwanza ya maombi hadi leo, kweli jina lako
libaeikiwe sana.
5. Bwana Yesu,
kama ulivyokuwa nami tangu siku ya kwanza ya maombi, leo naingia katika siku ya
kuvaa silaha za vita vya kiroho kwenye
maombi yangu katika jina la Yesu.
6. Baba Mungu
katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti naomba ukanitie nguvu zitokazo juu, ili
nipate kupambana na kumshinda huyu mwovu shetani, nipe ujasiri mwingi wa
kuwashinda kabisa mapepo wote wanaofuatilia mafanikio yangu ya kiuchumi.
7. Ndani yako ninalizamisha kila gari au chombo
nitakachotumia safarini kibiashara au vinginevyo, pia nawafunika madereva na
abiria wote kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti (tamka mara
3).
8. Adui zangu
wote nawatosa ndani ya moto wa Roho Mtakatifu wakakose amani mpaka watakapotubu
na kuliita jina la BWANA wa majeshi.
9. Kwa ngao ya imani nazuia kila mshale
unaorushwa na adui na kuuamuru umrudie aliyeurusha na kumdhuru kabisa katika
jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
Roho
Mtakatifu mwenye nguvu zote kwa nguvu zako nikomboe na kuniweka huru kabisa
katika jina la Yesu.
10. Ninamwagia damu ya Yesu juu ya kila kioo cha
kichawi wanachotumia kuniwinda na ninaamuru moto wa radi kutoka mbinguni
ukakivunje vunje katika jina la Yesu (rudia mara saba).
11. Kwa nguvu ya damu ya Yesu ninafuta madhara
yote ambayo yameandaliwa kuzimu kwa ajili yangu mwaka huu nayakanyaga katika
jina la Yesu.
12. Nafunga roho ya vizuizi vya kiuchumi, nafunga
roho ya kukopakopa, nafunga roho ya madeni,
nafunga roho ya chuma ulete, nafunga na kusimamisha roho ya kupoteza pesa na
mali katika mazingira ya kutatanisha, nafunga na kuvunja roho ya matumizi ya
hovyo hovyo, nafunga roho zote za kufikiria na kuamua kufanya biashara au kazi
yoyote isiyokuwa na faida na pia nafunga roho zote za kutapeliwa zinazotoka
kuzimu katika jina la Yesu.
13. Wewe pepo
la umaskini na ujinga, piga kelele na uondoke pamoja na roho
zote za
kutofanikiwa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
Baada ya
kuomba maombi haya tumia dakika saba kumshukuru Mungu
Tarehe ya
kuja kupokea maombi mengine na maelekezo ya kinabii ni ………………………. saa moja
asubuhi ukiwa umefunga ili upakwe mafuta. Ukimtii Nabii wa Mungu utafanikiwa.
Mimi wako
Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC Tabata Chang’ombe. Simu. 0756-863528. Amen.
Mwanamaombi namba ……………
-----------------------------------------------------------------------------------------
MWAMINI
MUNGU UTHIBITIKE, AMINI NABII UFANIKIWE (2 NYAKATI 20:20)
MAOMBI YA
VITA YA SIKU 21 ZA KINABII ZA KUFUNGA NA KUOMBA
Maombi haya
ya kinabii ni ya wiki 21, siku 21 na kila wiki ni siku 1 tu ya kufunga na
kuomba. (Ombi la kwanza 1). Hakikisha umesoma maandiko haya kabla ya maombi.
Amen
Kumbukumbu 28:1-14; Waefeso 6:10-18; Yeremia
1:10; Ayubu 42:2-10;
Mathayo
7:7; Luka 18:1; Nehemia13:2; Zaburi 103:1-5.
1. Baba Mungu
katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti naomba,
2. Nikiinua
macho yangu ili nipate kibali kutoka kwako wewe uliye Bwana wa majeshi, Mwamba
wa milele, nikikusifu na kukuabudu wewe, Nakuheshimu wewe ni katika jina la
Yesu.
3. Siku ya leo
ni ya hatari sana, ni siku ambayo nahitaji nguvu zako na ulinzi wako kutoka juu
katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
4. Naliinua
jina lako wakati huu ninapopigana vita hii takatifu katika jina la Yesu
5. Tamka moto
wa Roho Mtakatifu (rudia mara 7), Damu ya Yesu (rudia mara 7).
6. Baba Mtakatifu
katika jina laYesu ninakuja kwako na kupokea damu ya Yesu ikatakase nafsi yangu
na mwili wangu.
7. Kama
ilivyoandikwa katika Isaya 54:17
kuwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, natamka kwamba silaha
yoyote ya kichawi iliyo kinyume nami ishindwe na kuharibika katika jina la Yesu
Kristo.
8. Mishale
yote yenye moto ya yule muovu iliyotengenezwa kwa ajili yangu ikamrudie na
kumharibu aliyetuma katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
9. Ninawafunga,
kuwavunja na kuwaharibu kabisa mapepo wote waliotumwa mwaka huu kwa ajili ya
kusababisha ajali mbalimbali (tamka mara 3).
10. Popote ambapo jina langu limefichwa kichawi,
kimashetani, natuma moto usio wa kawaida mahali hapo na popote ambapo fedha
zangu na mali zangu zimezuiliwa katika ulimwengu wa roho, natuma moto Roho
Mtakatifu ateketeze nira na vifungo vyote katika jina la Yesu Kristo (rudia
mara 2).
11. Kama ilivyoandikwa katika Mithali 18:10 kuwa jina la BWANA ni ngome imara na mwenye haki
huikimbilia na kuwa salama, natamka usalama ulio katika Kristo Yesu popote
niingiapo, popote nitokako na popote nilipo.
12. Tena ninawafunga wachawi wote wanaoshambulia
maisha yangu, fedha yangu na mali zangu katika jina la Yesu.
13. Nakuita Ee Mungu wa Eliya uliyejibu kwa moto,
sasa tawala mahali popote penye uchumi, na mali zangu zilipofichwa na kukaliwa
vikao vya kichawi juu yangu katika jina la Yesu.
14. Ndani yako ninalizamisha kila gari au chombo
nitakachotumia safarini kibiashara au vinginevyo, pia nawafunika madereva na
abiria wote kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti (tamka mara
3).
15. Adui zangu wote nawatosa ndani ya moto wa Roho
Mtakatifu wakakose amani mpaka watakapotubu na kuliita jina la BWANA wa
majeshi.
16. Kwa ngao ya imani nazuia kila mshale
unaorushwa na adui na kuuamuru umrudie aliyeurusha na kumdhuru kabisa katika
jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
17. Roho Mtakatifu mwenye nguvu zote kwa nguvu
zako nikomboe na kuniweka huru kabisa katika jina la Yesu.
18. Ninamwagia damu ya Yesu juu ya kila kioo cha
kichawi wanachotumia kuniwinda na ninaamuru moto wa radi kutoka mbinguni
ukakivunje vunje katika jina la Yesu (rudia mara saba).
19. Kwa nguvu ya damu ya Yesu ninafuta madhara
yote ambayo yameandaliwa kuzimu kwa ajili yangu mwaka huu nayakanyaga katika
jina la Yesu.
20. Nafunga roho ya vizuizi vya kiuchumi, nafunga
roho ya kukopakopa, nafunga roho ya madeni, nafunga roho ya chuma ulete, nafunga
na kusimamisha roho ya kupoteza pesa na mali katika mazingira ya kutatanisha,
nafunga na kuvunja roho ya matumizi ya hovyo hovyo, nafunga roho zote za
kufikiria na kuamua kufanya biashara au kazi yoyote isiyokuwa na faida na pia
nafunga roho zote za kutapeliwa zinazotoka kuzimu katika jina la Yesu.
21. Wewe pepo la umaskini na ujinga, piga kelele
na uondoke pamoja na roho
zote za kutofanikiwa katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
Baada ya kuomba maombi haya tumia dakika saba
kumshukuru Mungu
Tarehe ya kuja kupokea maombi mengine na maelekezo ya
kinabii ni …………………… saa 2 asubuhi ukiwa umefunga ili upakwe mafuta. Ukimtii Nabii
wa Mungu utafanikiwa.
Mimi wako Nabii na Mtume wa Urejesho Peter Nyaga, RGC
Tabata Chang’ombe. Simu. 0756-863528. Amen.
Mwanamaombi
namba ………………
Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,
JibuFutaKwaheri Gerd Ulrich
Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
JibuFuta*penda uchawi
* kama unataka ex wako nyuma
* Acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa ulinzi
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159
Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
JibuFutaAnasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
*Kama unataka kupata mimba.
*Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
*Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
*Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
*Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
*Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159