MTUME NYAGA HR

AGALIA EMMANUEL TV LIVE [WATCH EMMANUEL TV LIVE]

Jumanne, 13 Mei 2014

MTUME PETER NYAGA AZAWADIWA MBUZI ZA NGUVU BAADA YA KUMALIZA MKUTANO MOROGORO

Kwa Yesu kuna raha ya ajabu. Ukifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu, Mungu aweza kukushangaza kwa muujiza wa ajabu sana. Waweza kufanya kazi ya Mungu bila ya kutegemea kupata kitu, lakini Mungu aweza kumtumia mtu au kitu chochote kukupongeza. Unapofanya kazi ya Mungu usifanye kama unafanya biashara, ila fanya kazi ya Mungu kama vile unapofanya kazi za ndugu yako.

Hii imemtokea Mtume Peter Nyaga baada ya kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu mkoani Morogoro, mkutano ulioandaliwa na Mwinjilisti Jailos Maloda, Mungu aliweza kuwatumia maasai ambao walijitokeza na kusema wamebarikiwa sana na mahubiri yake na hii iliwafanya watoe mbuzi za nguvu kama zwadi kwake.

Kwa kupitia ushuhuda huu unajifunza nini mtu wa Mungu?  Mtume Peter Nyaga wakati anatokea Dar es Salaam hakutegemea kupokea mbuzi lakini baada ya kumaliza kazi ya Mungu aliweza kupokea ujira wake. Nachotaka kusema kwako ni kwamba, FANYA KAZI YA MUNGU KWA UAMINIFU NA JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA KUFUATA AMRI KUMI ZA MUNGU







Tangazo limetegenezwa na Rumafrica +255 715 8515123

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...