Kutoka RGC Miracle Centre Tabata Chang’ombe
Mtume Nyaga agusa moyo wa jamii Dar
Mitume Manabii watikisa jiji wiki hii
Ishara, maajabu na miujiza vyatawala madhabahu ya RGC
Wengi wapiga kambi kanisani kuwahi vipindi
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida viti ndani ya ukumbi wa kanisa la RGC Miracle
centre Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu vimekuwa
vikikosa mkaliaji kutokana na wahudhuriaji kusikiliza mahubiri wakiwa
wamesimama kwa sababu ya upako unaotawala ndani ya nyumba hiyo ya ibada
wakati wa kongamano la kihistoria la siku 40 linaloendelea ndani ya
kanisa hilo.
Licha ya kongamano hilo la kihistoria kuchukua muda
mrefu, lakini idadi ya watu wanaomiminika kanisani hapo kuhudhuria
kongamano imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hali ambayo imekuwa
ikiwashangaza wengi.
Mbali na ishara, miujiza na maajabu
kutawala eneo hilo, jambo jingine ambalo limeonekana kuwavutia na
kuwashangaza wengi ni hatua ya kiongozi wa kanisa hilo mtume Peter
Nyaga, kuamua kuanzisha program maalum ya mafunzo ya ujasiriamali ambayo
imeonekana kuvuta watu wengi hasa wenye kipato cha chini na wasio na
ajira .
Wengi waliohudhuria mafunzo hayo walimshukuru na kumsifu
mtume Nyaga, kwa ubunifu wake kwani wanaamini pindi watakapofika mwisho
wa mafunzo hayo ya siku 40 yatakuwa msaada mkubwa katika maisha yao.
Walisema hii ndiyo sababu iliyowafanya wengi wao kuamua kuhama majumba
yao na kupiga kambi kanisani hapo ili kuhakikisha hawakosi kipindi hata
kimoja.
Tangazo limetengezwa na RUMAFRICA
Jambo jingine lililosifiwa na wahudhuriaji mbali na mafunzo ya
ujasiriamali ambayo yanaonekana kuwakomboa wengi tangu yalipoanza ni
hatua ya mtume Nyaga, kuwaleta watumishi wa Mungu kutoka madhehebu
tofauti kwa ajili ya kuwahudumia kiroho baada ya mafunzo ya ujasiriamali
jambo ambalo walisema ni la kipekee hasa katika kipindi hiki ambapo
ushirikiano miongoni mwa watumishi wa Mungu unaonekana kupungua nguvu.
Pia
katika kuendeleza kuboresha maisha ya watu wanaobahatika kuhudhuria
kongamano hilo la kihistoria, wiki hii mtume Nyaga, amealika wataalam wa
afya kutoka nchini Malaysia ambao watafundisha nguzo nne muhimu za
kuishi maisha mazuri na yenye afya bora.
Je unajua magonjwa haya yanasababishwa na nini mwilini mwako?
*Saratani ya utumbo mkubwa
*Vidonda vya tumbo
*Shini kizo la damu |
*Kisukari |
*Kufunga na kukosa choo mara kwa mara
*Figo kushindwa kufanya kazi vizuri
*Matatizo ya moyo
*Kukua kwa tezi ya prostrate (Prostrate gland)
*Kihararusi/Stroke
*Ngiri
*Magonjwa ya ngozi
*Unene uliopindukia
*Lehemu/ Cholesterol
*Harufu mbaya mdomoni na kikwapa
Usikose RGC Miracle Centre wiki
hii, kwani wataalam hawa waliobobea watakufundisha namna ya kuwa na
afya bora huku watumishi mbalimbali wenye upako wakikuombeea na
kukufungua kutoka katika vifungombalimbali vya shetani vilivyokutesa kwa
muda mrefu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni