Watu wamemiminika kama mvua katika mkutano unaoendelea katika viwanja vya K/Ndege mkoani Morogoro siku ya Jumatatu. Watu wamefika pale mapema sana kupokea ujumbe wa Yesu Kristo kwa kupitia watumishi hawa wawili yaani mwinjilisti Jailos Maloda wa Morogoro na Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Dar es Salaam. Idadi ya watu waliokoka kwa makadilio inasemekana ni kama watu 200 waliofika mbele ya jukwaa na kuungama dhambi zao mbele ya maelfu ya watu na kukiri kuwa walikuwa wakosaji na sasa wameyakabidhi maisha yao kwa Bwana Yesu Kristo.
Katika kutano huu kulikiwa na waimbaji mbalimbali kama vile Masanja Mkandamizaji, Mess Jacob Chengula, Joshua Makondeko na wengine weni ambao kwa kupitia karama zao za uimbaji waliweza kugeuza mioyo ya watu na wakampokea Bwana Yesu Kristo siku hii ya Jumatatu
Mtume Peter Nyaga akisalimiana na mwimbaji wa nyimbo za injili Joshua Makondeko
Mtume Peter Nyaga akisalimiana na Masanja Mkandamizaji
Mtume Peter Nyaga (kushoto) akiwa na Mess Jacob Chengula
Mess Jacob Chengula akijiweka sawa kwa kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji
Msanja Mkandamizaji akiwaleta watu wa Mungu kwa Bwana Yesu kwa njia ya uimbaji