MTUME NYAGA HR

AGALIA EMMANUEL TV LIVE [WATCH EMMANUEL TV LIVE]

Jumanne, 2 Julai 2013

MKUTANO WA KUOMBEA AMANI SIKU YA LEO WAPAMBA MOTO KATIKA KANISA LA RGC TABATA CHANG'OMBE KWA MTUME PETER NYAGA: NABII LIVINGSTONE NA MTUME JOSHUA WATIMUA VUMBI LA UPAKO WAKISINDIKIZWA NA WAIMBAJI KAMA MIRIAMU LUKINDO

Mkutano huu ni ulizinduliwa rasmi siku ya jana na Mtume Dk. Vernon Ferdnandes wa AGAPE siku ya jana. Mtume aliweza kufungua kwa maombi na aliweza kuhubiri injili. Watu walibarikiwa sana na huduma yake. Mtume Vernon aliongozana na mke wake kuhakikisha kazi ya Mungu inafanyika. Pia jana Nabii Joshua Tumba kutoka Afrika Kusini aliweza kuhubiri.

Waimbaji mbalimbali walikuwepo siku ya leo akiwemo Miriam Lukindo, makondeko, Kinyatta na Praise Team ya kanisa la RGC hapa Tabata Chang'ombe. Waimbaji walitwala jukwaa kwa kishindo kikubwa sana. Mungu alionekana mahali pale kwa njia ya sifa.

Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC hapa Tabata Chang'ombe ambaye ni mwenyeji wa mkutano huu aliweza kufungua mkutano kwa njia ya maombi na aliweza kuhubiri Neno la Mungu. Watu walionekana kubarikiwa sana kwani kulikuwa na nguvu za Mungu kwa wale waliojiachia kwa Mungu

Mtume Peter aliweza kuwakaribisha waimbaji binafsi ambapo kila mwimbaji alipata muda wa kutosha wa kumuimbia Mungu, Waimbaji hawa walikonga sana mioy-o ya watu kwa uimbaji. Watu wa kwanza kumuimbia Mungu walikuwa wenyeji wa kanisa hili la RGC hapa Tabata Chang'ombe ambao wanaenda kwa jina la Praise Team, na baada ya hapo walifuat0ia waimbaji wengine kama Miriamu Lukindo, Makondeko, Kinyatta na wengine wengi

Baada ya sifa kumalizika Mtume Nyaga aliweza kumkaribisha mtumishi wa Mungu, Nabii na Mtume Livingstone kwaajili ya kuwaombea watu na kuwatabiria maisha yao. Nabii na Mtume Livingstone aliwatabiria na kuwaombea watu na haya ni baada ya yale aliyohubiri siku ya leo,

"Tussome katika kitabu cha Ezekiel 47:1-12: na somo letu ni KUMILIKI BILA YA KIPIMO

Ninasema wanakuloga ninaomba wasife haraka bali wafe polepole, maana nataka waweze kuonba baraka za Yehova zinavyoshuka katika maisha yako.

Mungu anasema magoti yako ninapaka mafuta, maombi yako unayoyaomba yote yatajibiwa na Mungu. Sasa shika magoti yako. Maombi yako yanaleta matunda kwani Yehova anajibu sasa. Ukiomba Jumanne nanajibu Jumatano...Mwezi wa kawanza, wa pilio, nne, wa tano..nakuendelea maombi yako yatajibiwa.Ukiomba kiwanja, mke, nyumba, mafanikio, fedha, n.k, Mungu atakupa.

Ninakutabiria sasa ya kwamba mwaka 2013 ni mwaka wa kuzalisha. Utazaa watoto na wengine mapacha, biashara yako inaenda kuzaa biashara nyingine, kanisa linaenda kuzaa wafanyabiashara, wachungaji, waimbaji. Ninaitabiria Tanzania kuwa Tanzania utazaa amani, wahubiri wa kimataifa, waimbaji wa kimatafa. Ninasema hakuna umaskini tena ndani ya RGC Miuracle Center, watu wanaenda kubarikiwa na kuwa matajiri.

Kuanzia sasa upako unakuja kwako ni upako wa kubarikiwa bila ya kipimo, utainuliwa bila kipimo, utabarikiwa bila kipimo, utapakwa mafuta bila kipimo, utapokea uponnyaji bila kipimo, utapokea ushindi bila ya kipimo.

Waomshangilia Mungu wabarikiwa bila kipimo, ninaona baraka isiyopimika inashuka juu ya maisjha yenu. Ninasema kuna watu pesa zitaonekana usoni mwako. Pesa zitakutafuta mwenyewe. Kile ulichokuwa ukitafuta kinaanza kukutafuta. Hauna haja ya kuvaa suaruali ya kubana na ukawa kama kinyago kwa kuwatega waume za watu.

Ninawatabiria wamama kuwa kama una mume wako alipotea na kukuacha hatalala aliko huko, mabinti mliopo hapa mtapigwa harusi mpaka matumbo yenu yachomoke na mtapendeza sana, hakuna mwanaume atakkaye kukumbia tena. Aliyekuwa chini atakuwa juu.

Kuna watu 11 Mungu amenambia wamepata promosheni zao. Ninaona Ester ul;ikuwa ukiwaza bila ya majibu na sasa Mungu anaenda kukuinua.

KUTABIRI: Watanzania watapata pesa, kutakuwa na Investors wengi Tanzania. Ninasema Tanzani zaa matunda mazuri katika jina la Yesu. Ninaona baraka zimeshuka mikononi mwenu, kutakuwa na furaha, ushindi na amani..Amen."

Baada ya kumaliza kazi ya Mungu, Mtume Peter Nyaga alimwalika Nabii Joshua Tumba kutoka Africa ya kusini kwajili ya kazi ya Mungu. Nabii Joshua alimshukuru Mungu sana kwa kumuwezesha kufika madhabahuni na aliweza kuhubiri injili. Alipomaliza kuhubiri aliweza kuwatabiria watu maisha yao ya kimafanikio. Watu wengi walitabiroiwa. Na haya ni baadhi ya yale aliyoyasema siku hii,

" Mungu hayuko kwa masaa mengi, anaweza kufanya kazi kwa dakika tano juu, ndio maana ninasema nyoosha mkno wako kwa Mungu. Kuna waytu wengine Mungu anawapa upako na wanaanza kuchezea, hawajui thamni ya upako ambao Mungu amewapa. Ninakuambia leo Mungu atakuwa na wewe. Mambo ya Mungu hayahitaji kulazimishwa ni Mungu tu anatenda


KUTABRIA
Kuna kitu huwa kinasimama sana kwako na unatamani kulia na kulia unalia kama mtoto

KUTABIRIA WAFANYABIASHA: Bwana Mungu wako atakufanya mwingi wa heri katika kazi ya mikono yako. Sasa wafanyabiashara shika kitovu chako, kwani Mungu anauwezo wa kubadilisha kiwanda cha palachichi na kuwa kiwanda kikubwa sana. Ninakuambia Bwana atafurahi juu yako kwani utafanikiwa sana. Ninakutabiria kama kamandawa vita. Ninasema nikija tena hapa kwa Mtume Nyaga nitatabiri na watu watakuwa na magari

MAMA TABAIRIWA JUU YA KUFA GANZI MKONO WAKE: Kuna mama mkono wake unakufa ganzi na hii ni roho ya mauti. Baba ninaachilia upako ninaomba uje mbele.

Tusome Torati:11:24: Kila mahali utakapokanyaga tu hata kwa kutembea na kwa nyayo za migfuu yako patakuwa pako. Ninasema Kongo, Afrika kusini utakanyaga na mpka bahari ya magharibi itakuwa mipaka yenu.

Sasa ninataka nikuombee wewe mfanyabiashara, ninaomba unyooshe mkono wako sasa, "Baba ninaomba ukawabariki watu wako, kabariki mikono yao, kabariki kazi zao. Mungu ukawalinde na kuwawezezesha kwa jina la Yesu. Amina"

Mwisho: Mtume Peter Nyaga aliweza kufunga kwa maombi na kuwatakia watu wote waliofika mahali hapa na wale waliokuwa wakisikiliza kwa njia ya radio, TV na waliokuwa wakiangalia kwa njia ya faceboo na blogu ya kanisa hili www.urejeshotv.blogspot.com, aliwatakiwa mafanikio mema na kuwaalika tena siku ya kesho.


Mungu akubariki sana

Mpiga picha na mwandishi ni Mkurugenzi wa Rumafrica. Tembelea blogu yetu

www.rumaafrica.blogspot.com

www.rumaafricajobs.blogspot.com

www.tbjoshuarumaafrica.blogspot.com

Simu: +255 715851523

KIPINDI CHA SIFA NA KUABUDU
Waimbaji wakiwa kazini siku ya leo



Miriamu Lukindo




MIRIAMU LUKINDO AKIWASHA MOTO KWA NJIA YA SIFA


Kulia ni Miriamu Lukindo katika sifa


























MAKONDEKO AKIWASHA MOTO WA SIFA KATIKA MKUTA HUU SIKU YA LEO







































PRAISE TEAM WAKIWA MADHABAHUNI KUMUIMBIA BABA YETU WA MBINGUNI SIKU YA LEO

Mwalimu wa Praise Team akiongoza sifa




















MTUME PETER NYAGA AKIFUNGUA MKUTANO WA LEO KWA NJIA YA MAOMBEZI NA PIA AALIFUNDISHA NENO LA MUNGU





Mtume Peter Nyaga akiombea Taifa na kufungua mkutano kwa siku ya leo







Mtume Peter Nyaga akifungua mkutano kwa maombi

Mtume Peter Nyaga akiwa na Praise Team



Mtume Peter Nyaga




MWIMBAJI YA INJILI KUTOKA KENYA KINYATTA ALIWEZA KUMSIFU MUNGU SIKU YA LEO NA HIVI NDVYO ALIVYOFANYA KWA UTUKUFU WA MUNGU.

Kinyatta kutoka Kenya





Mtume Nyaga akiteta jambo na Mtume na nabii livingstone
























MTUME PETER NYAGA AKIMKARIBISHA NABII NA MTUME LIVBINGSTONE




NABII NA MTUME LIVINGSTONE AKIHUBIRI NA KUTABIRI MAISHA YA WATU
























































Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...